Tuesday, 23 July 2013

'NASUMBULIWA NA FANGASI SEHEMU ZA SIRI....TATIZO LILIANZA MWAKA 2008."...NAOMBA USHAURI WA MATIBABU


By on 21:53

Huyu ni mtanzania mwenzetu ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuwasha sehemu zake za siri.Leo ameamua kuziweka  aibu  pembeni  na  kulianika  tatizo  lake  akiamini  kuwa  jamii  itamsaidia  KIMAWAZO.
-------------------

HUU NI UJUMBE WAKE:
Mficha maradhi mauti humuumbua.Mdogo wangu wa kiume amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuwasha sehemu zake za siri tangu mwaka 2008.Ilifikia hatua korodani zake zikabadilika ngozi na kubabuka kama za mbwa na zikawa zinatoa harufu.

Hapo hakuwa na jinsi zaidi ya kunieleza.Nilichokifanya ni kumpeleka hospitalini.Walipima damu yake, mkojo, ngoma, kinyesi lakini hawakuona kitu.Walimpa dawa za kutumia kwa muda alafu aone kama zitamsaidia.

Zile dawa hazikutibu chochote.kwa kiasi fulan, zilisaidia kuikausha ngozi lakini baada ya muda hali ilirudi kama zamani.

Nimezunguka naye sana bila mafanikio.hata dawa za kienyeji katumia pia lakini hakuna kitu.

Jamani, kama kuna mtaalam yeyote tunaomba atusaidie kimawazo.Tufanyaje ili kulitibu tatizo lake?

Je, hii ni fangasi au ni gonjwa gani.


Asanteni.
Noni.

About Syed Faizan Ali

Faizan is a 17 year old young guy who is blessed with the art of Blogging,He love to Blog day in and day out,He is a Website Designer and a Certified Graphics Designer.

0 comments:

Post a Comment