Tuesday, 23 July 2013

POLISI WAFANIKIWA KUMKAMATA MVUTA BANGI ANALIYEMUUA MDOGO WAKE KWA KUMKATA MAPANGA HUKO SINGIDA


By on 22:07

 Jeshi la polisi mkoa wa Singida limefanikiwa kumkamata Elibariki Alphoce (21) mkazi wa kijiji cha Kizega wilaya ya Iramba, anayetuhumiwa kumuua mdogo wake Mariam (9) mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Kizega.

Elibariki anatuhumiwa kumuua mdogo wake Mariam Julai 16 mwaka huu katika kijiji cha Kizega kwa kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili na kisha kuteganisha kichwa na kiwiliwili.

Ilielezwa kuwa Elibariki ni mtumiaji sugu wa madawa ya kulevya aina ya bangi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Julai 18 mwaka huu akiwa amejificha kando kando ya mto Ruruma wa kijiji cha Ruruma tarafa ya Kiomboi.

About Syed Faizan Ali

Faizan is a 17 year old young guy who is blessed with the art of Blogging,He love to Blog day in and day out,He is a Website Designer and a Certified Graphics Designer.

0 comments:

Post a Comment