Diouf ambaye alikiri kutumia madawa hayo toka mwaka 1996 alisema alikata shauri mwenyewe na kwenda kutibiwa kwenye hospitali ya Lutindi iliyopo Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
“Nilianza kubwia unga toka mwaka 1996, sikujua
kama unga una madhara, awali nilikuwa navuta bangi lakini kuna jamaa
mmoja sasa hivi ni marehemu ndio alinifundisha kubwia unga.”
“Kuna wakati alikuwa anachanganya unga na bangi.
hata hivyo mimi na wenzangu hatukujua kama anachanganya na bangi, kuna
siku akatupa bangi bila ya kuchanganya na unga tulivyovuta tukaona mbona
ipo tofauti na haileti ulevi sana, tukamuliza hii vipi mbona mbaya
akasema sijawachanganyia, tukamuuliza hujatuchanganyia na nini akasema
unga, tukamwambia tuchanganyie basi, kweli alipochanganya tukavuta
tukajiona kama tuko Ulaya vile, dunia yote ipo mikononi mwako.”
“Kuanzia hapo ndio nikafungua ukurasa mpya wa
kutumia dawa za kulenya, nikafikia kipindi nikaacha kuchanganya na
bangi, nikawa nabwia na kunusa, wakati ule kete moja ilikuwa ikiuzwa
Sh250 sasa hivi inauzwa Sh2,000.”
“Uteja ni kitu ambacho kinaweza kukudhoofisha,
mimi ulikuwa ukinidhoofisha kwani nilikuwa siwezi kupanda stejini kuimba
kama sijabwia, nilikuwa mteja msafi, kipindi cha mwazo watu walikuwa
hawajui kama mimi ni teja, ila wale wa karibu wakawa wananiambia mbona
sauti inabadilika kama inakwaruza na kukauka.”
“Ilifika wakati mwili ulidhoofu, Diofu wa leo sio
yule sasa hivi nina afya hata wewe si unacheki, nilikonda sana nilifikia
hatua nikawa nikilala saa 10 usiku tunapomaliza kuimba siamki mpaka saa
moja usiku, na nikiamka nakula kisha lazima nibwie ndio nitajisikie
freshi.

ILIKUWAJE AKAACHA:
“Unajua mwanzoni mke wangu na ndugu zangu walikuwa
wakinikamata kwa nguvu na kunipeleka hospitali, basi nikajikuta naacha
na kurudia, sikuwahi kuacha moja kwa moja kama ilivyo sasa.”
“Nina watoto wawili, Najma a.k.a Vannesa na Taslim
a.k.a Paris’ sasa roho iliniuma sana siku moja watoto wenzao walikuwa
wanawaambia baba yenu nyie ni teja.
“Nilijisikia vibaya kuona watoto wangu watazidi kusakamwa kwa kuambiwa kuwa baba yao (mimi)ni teja.
“Hali hiyo ndio iliyonifanya niamue kukata shauri na kwenda Muhimbili nikaonana na Dokta Ayubu ambaye yeye akanipeleka Lutindi, hiyo ilikuwa ni mwaka jana na nilikaa hospitali kwa miezi mitatu lakini toka nimetoka huko nina miezi tisa na bado naendelea kupata ushauri Muhimbili, huwa naenda kila Jumatano na Ijumaa.”
“Hali hiyo ndio iliyonifanya niamue kukata shauri na kwenda Muhimbili nikaonana na Dokta Ayubu ambaye yeye akanipeleka Lutindi, hiyo ilikuwa ni mwaka jana na nilikaa hospitali kwa miezi mitatu lakini toka nimetoka huko nina miezi tisa na bado naendelea kupata ushauri Muhimbili, huwa naenda kila Jumatano na Ijumaa.”
WASANII KUPOTEZA MAISHA KWA AJILIYA UNGA
“Wasanii wengi wanatumia dawa za kulevya, wengi nimewaona wamedhoofika, namshukuru Mungu kwa kunitoa katika janga hilo.”
ALIJISIKIAJE ALIPOFIKA HOSPITALI KWA MARA YA KWANZA
“Sio siri unga unatoka mwilini kwa saa 72 yaani
siku tatu, na ndio maana ukikosa kutumia siku moja tu lazima utaharisha
sana na kutapika, utatetemeka kama mgonjwa wa malaria na unaweza
kupoteza maisha usipopata, ndio maana ukishabobea wengine wanakuwa
maskini, kwa sababu upo tayari kuuza chochote mradi upate hela ya
kununua unga.”
“Mimi nilipofika Lutindi nilipatwa na hali hiyo
sana, nikawa napiga kelele kama kichaa, yaani unaomba wakupe hata kidogo
tu, lakini walichokuwa wanafanya ni kunichoma sindano ya usingizi maana
bila sindano huwezi kupata usingizi.
Huko Lutindi sikuwa peke yangu, nilikuta watu
kibao huko wengine walikuwa wameathirika mno hasa wale waliokuwa
wakijidunga sindano, mimi namshukuru Mungu sikufikia kujidunga.”
ANASHAURI NINI WASANII WENZAKE:
“Wasanii ambao wanatumia unga wanitafute namba
yangu ni 0777 926111 kama kweli kuna ambaye anataka kuacha kutumia unga
kwa hiyari yake tena, nawahakikisha ataacha bila hata ya kuumia” anasema
Diouf huku akionekana kujutia kujiingia kwenye vitendo hivyo vya ulevi.
ASHA BARAKA ANAMZUNGUMZIAJE DIOFU?
“Diouf bado ni mfanyakazi wa Asset, na moja ya
mikakati ya Kampuni yetu si tu kuwatumia wasanii bali pia kuwajali afya
zao, mara nyingi tumekuwa tukimsaidia katika matibabu yake mara kwa mara
na sasa hivi vita yetu kubwa tunayopigana nayo ni kuhakikisha anaacha
kunywa pombe.
“Ugomvi wetu sasa hivi kwa Diofu ni pombe tu,
naamini akiacha Pombe hata matibabu yake atayafanya vizuri zaidi na ndio
maana tumemsimamisha mpaka kwenye maonyesho yetu ili apate matibabu
yake vizuri.”
Baraka anasema kuwa licha ya kumsimamisha kwenye
maonyesho yao wamekuwa wakimpa stahiki zake zote ikiwemo posho na
kumpongeza rapa huyo kuwa balozi mzuri wa vijana katika kupiga vita dawa
za kulevya nchini.
“Aisha Madinda aliingia kwenye huo mkumbo, akatoka
bendi yetu na kwenda bendi nyingine, tumemsaidia sasa hivi anaendelea
vizuri, tupo kwenye mpango wa kumrudisha Twanga, na safari hii sio tu
atanengua, pia atajifunza mambo mengine kama uimbaji na vitu
vingine,”anasema.
Aisha Madinda ambaye ni mnenguaji wa bendi ya
Extra Bongo, baada ya kutumia dawa za kuondoa sumu hivi sasa ni
muhamasishaji kwa ‘mateja’ ambao bado wanatumia ‘unga
Madinda alikaririwa siku za hivi karibuni akisema bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia amepewa kazi ya uhamasishaji katika Shirikia la Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Ukimwi (PHRP) lililopo Kinondoni.
Madinda alikaririwa siku za hivi karibuni akisema bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia amepewa kazi ya uhamasishaji katika Shirikia la Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Ukimwi (PHRP) lililopo Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment