Tuesday 30 July 2013

BODI YA MIKOPO YAKANUSHA UVUMI KUWA WALIOOMBA MKOPO WA ELIMU WANAPASWA KUJIANDIKISHA UPYA



Kumekuwa na uvumi kwamba mtandao wa uombaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (OLAS) ulikuwa na hitilafu ya kiufundi na hivyo Wanafunzi wanaondelea na masomo ambao walikuwa tayari wameshahakiki taarifa zao wanapaswa kurejea kujaza upya ama kuhakiki iwapo taarifa zao zipo mtandaoni.

Bodi inatumia fursa hii kuwajulisha Wanafunzi husika, Vyuo vya Elimu ya Juu na Umma kwa ujumla kuwa taarifa za Wanafunzi hao zilizopokelewa ziko salama na hawapaswi kujaza tena na hivyo taarifa hizo za uvumi zipuuzwe.

Aidha Bodi inasisitiza kwamba kesho tarehe 31 Julai, 2013 ni


mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ya waombaji wote wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.

Bodi inawapa nafasi ya mwisho waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: http://olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti: www.heslb.go.tz

Tangazo hili limetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU.

"SINA MPANGO WA KUAJIRIWA NA KU******M YOYOTE....CLOUDS ACHENI KUNIFUATILIA". HILI NI TUSI LA MWISHO MWAMPAMBA



Mwisho Mwampamba amegeuka  mbogo  na  kufurumua  matusi  ya  nguoni  kwa  Clous Fm  baada  ya  kituo  hicho  kuanza  kumjadili  na  kumchambua...

Mwampamba, ambaye  ni  staa  namba  mbili  wa  shindano  la  big  brother  mwaka  2003  anadai  kutoridhishwa  na  kitendo  cha  Cloud  fm kuanza  kumjadili...

Staa  huyo  amedai  kwamba  yeye  anamaisha  yake  na  hivyo  haoni  haya  ya  kuanza  kufuatiliwa  kwa  kuwa  hana  mpango  wa  kuomba  ajira  kwa  yeyote...

"Clouds fm siwaelewi mnatafuta nini . Nahisi mnatafuta kupakazwa mafuta ya ubuyu . Tafadhali kusaga naona heshima inapungua . 


"Had mifugo yako hujawalea vizuri . Mimi sio msanii na pia sita ajiriwa na k**ma wowote yule . Stay away from me n my family.Ameandika  staa  huyo  katika    account  yake  ya  facebook

KODI YA SIMU KURUDI BUNGENI AGOSTI MWAKA HUU KWA AJILI YA KUJADILIWA UPYA



SAKATA la kodi ya simu ya Sh 1,000 kwa kila laini ya simu kwa mwezi, inayolipwa na watumiaji wa simu, litamalizwa bungeni kisheria. 


Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesema wameanza kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete, la kuitaka Wizara ya Fedha kukutana na wadau wengine, kuangalia namna ya kupata vyanzo vingine vya mapato mbadala wa kodi hiyo.



Alisema hayo alipozungumza jana na Habari leo, baada ya kusaini mkataba wa msaada wa zaidi ya Sh bilioni 344, kutoka Benki ya Dunia, ili isaidie masuala mbalimbali katika sekta ya usafirishaji. 
 
Mgimwa alisema katika suala hilo, masuala ya kisheria yatafikishwa bungeni mwezi ujao, ili kumaliza utata wa kodi hiyo.



Alisema uamuzi wa kushughulikia suala hilo, ulifikiwa kutokana na agizo la Rais Kikwete la hivi karibuni, kutaka wizara hiyo na ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kukaa na kampuni za simu kumaliza utata uliojitokeza kuhusu kodi hiyo.



Awali Umoja wa Wamiliki wa Kampuni za Simu (MOAT), ulitoa maoni kutaka kufutwa kwa kodi hiyo, kutokana na kulalamikiwa na wadau wa sekta ya mawasiliano.



Mbali na Moat, pia baadhi ya viongozi wa Serikali, wabunge na wananchi, walipinga kodi hiyo kwa walichokieleza kuwa itaongeza mzigo wa ugumu wa maisha kwa mtumiaji, hususan wa kipato cha chini.


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, alipozungumza na gazeti hili jana, alisema mara baada ya Rais kutoa agizo, wizara husika zilikutana kufanyia kazi agizo hilo.

"Rais akishaagiza kinachofuata ni utekelezaji na sisi kesho yake tulianza vikao na ninachoweza kukwambia tuko pazuri na tukikamilisha majadiliano yetu, tutatoa taarifa," alisema Makamba.



Alisema lengo ni kuangalia kama Serikali inaweza kupata Sh bilioni 178 kutoka vyanzo vingine, iwapo itaamua kufuta kodi inayotokana na tozo ya Sh 1,000 kutoka kwenye laini za simu.



Hivi karibuni, Rais Kikwete aliagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano na kampuni za simu za mikononi nchini, kukutana kutafuta jinsi ya kumaliza mvutano wa kodi hiyo.



Alitoa maelekezo hayo baada ya kukutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa kampuni za simu za TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel. 


Rais alisema lengo kuu la mkutano huo, liwe kupendekeza jinsi ya kuziba pengo la Sh bilioni 178 ambazo zitapotea katika bajeti, iwapo kodi hiyo itafutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/14.



Aliwaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa hawezi kuifuta moja kwa moja kodi hiyo, bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo litakalotokeza, huku tayari Bunge limezipangia matumizi.


“Nakuombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tutajaza pengo hili la Sh bilioni 178, endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,” alisema Rais Kikwete.

Habari Leo

Monday 29 July 2013

BAADA YA CLOUDS FM KUMWONGELEA MWISHO MWAPAMBA ,YE AKASIRISHWA NA KITENDO HICHO NA KUTOA TUSI ZITO LIVE


 Now ni clouds FM with Mwisho Mwampamba

WAKUTWA NA MAUTI WAKIFANYA MAPENZI.



Kwa Mujibu wa Ripoti iliyotolewa na wakazi wa eneo husika, inasemekana kwamba Bw. Mathias Nwoko,45, na Binamu yake Angela Ihuoma walifikwa na Umauti wakati wakiwa katika tendo la ndoa.
Wawili hao ambao asubuhi kabla ya kufariki walionekana pamoja wakicheza kwa furaha katika sherehe za kumkaribisha Padri Mpya katika Jimbo lao, Mathias ambaye ameelezwa alikuwa ndani ya ndoa kwa kipindi cha miaka 13 bila ya kupata mtoto alirudi na binamu yake usiku wakitokea kusikojulikana na kumkuta mkewe akiwa anaangalia T.V nyumbani kwake.
Mathias alimwambia mkewe atangulie kulala kwasababu yeye anachukua tochi amsindikize binamu yake huyo kwao. Mama mzazi wa Angela alipoona usiku unazidi na mwanawe hajarudi alimtafuta kupitia simu yake ya mkononi ambayo alipokelewa na Mathias akimwambia wapo pamoja.
Mpaka asubuhi, Si Mathias wala Angela Aliyerudi kwao na ndipo familia zote mbili zilipoingiwa na wasiwasi, Mke wa Mathias alienda katika nyumba yao ya pembeni asubuhi hiyo na ndipo alipowakuta wawili hao, mwanamke akiwa juu ya mwanaume.
Aliganda kwa muda asiamini anachokiona,hasa kuona wawili hao hawashtuki japo kawaona na ndipo alipogundua ya kwamba wamefariki Dunia. Ilibidi kutoa taarifa kwa familia ya Angela ambapo alikuja mama yake mzazi ambaye alipigwa na butwaa kutokana na picha iliyokuwa mbele yake.
Miili yao ilitenganiswa na kupelekwa hospitali huko Ogbor Nguru, jimbo la Aboh Mbaise.

TAARIFA KWA UMMA, BARABARA KUFUNGWA KWA UJUIO WA WAZUIRI MKUU WA THAILAND NCHINI TAREHE 30/07/2013




Ndugu Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Napenda nichukue fursa hii kuwajulisha rasmi kwamba Nchi yetu imepata heshima ya kutembelewa na Waziri Mkuu wa Thailand ambaye atawasili Nchini tarehe 30/07/2013. Ziara hii ni ya kikazi (state visit) na atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kumbukumbu ya Mwalimu J. K. Nyerere majira ya saa 6:30 mchana na kulakiwa na mwenyeji wake Mhe. Rais wetu mpendwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Mkoa.

Ndugu Wananchi,
Baada ya kuwasili Mhe. Waziri Mkuu wa Thailand atakagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na pia atapata fursa ya kukagua vikundi mbalimbali vya ngoma ambavyo vitakuwa vikitumbuiza na kutoa burudani kwa Mgeni wetu na msafara wake.
Ndugu Wananchi,
Mgeni wetu baada ya kukagua vikundi vya ngoma na burudani ataondoka kuelekea Ikulu kupitia barabara ya Nyerere, Railway, Gerezani, Sokoine Drive hadi Ikulu. Akiwa Ikulu atasaini mikataba mbalimbali kati ya Serikali ya Tanzania na Thailand. Usiku atashiriki katika dhifa maalumu iliyoandaliwa na Mwenyeji wake.

Endelea kusoma habri hii kwa kubofya hapa chini

Ndugu Wananchi,

Tunaomba radhi kwamba barabara hizi nilizozitaja zitafungwa kwa muda kupisha misafara ya Viongozi wetu Wakuu watakaoelekea Uwanja wa Ndege wa Kumbukumbu ya  Mwalimu J. K. Nyerere kumlaki Mgeni wetu hususan barabara ya Nyerere kuanzia saa 6.00 mchana hadi saa 7.30 mchana.

                       Ndugu Wananchi,
Tarehe 31/07/2013 Waziri Mkuu wa Thailand atatembelea Mbuga za Wanyama za Serengeti.Tarehe 01/08/2013 atarejea Dar es Salaam na kuagwa rasmi katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere na kuendelea na ziara yake huko Uganda.
Ndugu Wananchi,
Kama ilivyo ada tunaombwa kumlaki mgeni wetu kwa shangwe na bashasha katika maeneo yote atakayopita. 
Asanteni kwa kunisikiliza.
                  Saidi Meck Sadiki
                  MKUU WA MKOA
                  DAR ES SALAAM