Saturday 20 July 2013

BEEF YA MANGE KIMAMBI NA SINTAH HII HAPA (PARTY ONE)


By on 03:07




Haya yaliandikwa Tarehe 18 July na Mange Kimambi ndio yaliyo sababisha website yake kucrush kwa jinsi watu walivyoingia wengi kwa mara moja kwenye hiyo website...Haya jisomee Mwenyewe Gazeti hilo Hapo chini:

Uwii na yangu isije crush ..Slow down 

UKWELI WA MAMBO........


"I had a busy day leo mpaka basi ndo maana mnaona sikuapprove comments zenu. I was just sooooo busy...... Ila sasa hivi nimetulia nipo ndani ya ndege na familia yangu tukielea L.A. Ndo nkona niblogue sasa.

Unajua nini mwezi wa Ramadhan hamzuii mtu kusema ukweli  kwa hiyo acheni niongee.

Nimeoingia online tu natumiwa link nimeingia naona watu au hata labda inawezekana ikawa ni mtu mmoja tu kaandika zote si mnamjua yule hamnazo alivyo. Anyays, it doesnt matter kama comments kaandika mtu mmoja au wameandika wengi au kama Sinta mwenyewe kaandika ili watu wamwonee huruma sijui ila what matters is mtu ambae hajui kwanini nilifanya vile jana anaweza kuniona mimi ni mtu mbaya sana, nina wivu na wanawake wenzangu, ninawavunja moyo na kuwaharibia majina yao. Kwa kweli siwezi kukubali kuwa na kashfa kama hii sababu mimi ni mgombea mbunge mtarajiwa wa jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Ukweeeeeee ,CCM. Nimeona bora nijiteteee angalau.

Nawaomba sana baada ya kusoma ntakachokiandika ukipenda kutuma commnets tuma comments zenye busara na kujenga tafadhali usitume comments za kumdhalilisha mtu.

Like i said malalamishi yanatembea mimi nimeamua kumuumbua Sintah kwa kutangaza kuwa kachukua mkopo access bank sababu sijapendezewa na yeye kufungua duka, nina wivu etc. Naomba mjue kwamba huo sio ukweli hata kidogo.

Hizi taarifa za Sintah kuchukua mkopo nipewa kama mwezi au miezi miwili iliyopita kupitia mtandao wa FB na alinieleza kuwa amekasirishwa sana na comments ambazo bibie JLO TZ alikuwa ameweka siku hiyo kwa hiyo akanipa hiyo data ili na mimi nijibu mapigo. Nilimshukuru huyo dada kwa habari nilimshukuru sana sana mpaka kwa mapenzi aliyoonyesha kwangu sababu aliamua ku risk kazi yake sababu yangu mimi. Although kuna wanaoniona mimi ni mpenda ugomvi na kubully watu nilimweleza huyo dada sitaki kuweka hii habari sababu ni serious sana yeye maneno anayoniandika ni ya kitoto im sure watu wameshayazoea so nitamwacha aendelee.Nikakaa kimya.

Im sure wote mtakubaliana na mimi kuwa toka last time balaa lilivyozuka ikawa vita ya karibia wiki nzima nilisema sitaki ugomvi and i tried my very best to keep my word, Ila mwenzangu yeyee aliendelea kunidonyoa donyoa kidogo kidogon nikasema mwache ajifurahishe na hata siku moja sikuweka comment humu kuhusu yeye sababu mimi nikishamdharau mtu yani huwa nasahau kama yupo hai.

Huyu SInta ananitafuta kwa shari on a daily basis, yani hanipi hata day off mutoto wa kike. Alikuwa anadiriki mpaka kuweka comments za link kuwaonyesha watu eti kuwa nguo zangu nanunua naweka label, anaweka comments vitenge vyake ni feki. Akawa anaweka comments za BEDUI Mange anaishi hapa kwenya watu maskini, hivi ile address ingekuwa kweli ni yangu ningedhuriwa je? We all know how much BEDUI hates me ,angekuwa nauwezo angesha hire hitman animalize. Nikaenda zangu L.A mwenyewe nikaona nijishebedue mnione babkubwa nikaenda kwa jirani yangu nikapiga picha ndani kwake nikawaekewa, mkanisifia weeee, mara akaweka comment za kuniumbua  kuwa nakaa kwenye ki apartment , maneno kibao.aliniumbuaje sasa??? LOL...

Mnakumbuka nilivyokuja US nikaweka porche yangu nawaringishia, bidada akarusha macomment gari yenyewe ya mkopo, akawa kila akipiga picha chini anaandika siishi kwa mkopo. Maskini nilikosaje raha kaniumbua gari la mkopo. Imagine mpaka alidiriki kuweka comments kuwa muke ya muzungu mimba imeingia chooni. Imagine wakati anaweka hii comment taayri nilikuwa najua mambo ya mkopo na nilikuwa nakumbuka anavyosema haishi kwa mikopo lakini stili nilijikaza nikasema bwana eeeh mwache kila mtu ananijua mimi taifa kubwa sina haja ya kumjibu.  Sasa alivyofungua duka ndo akadata kabisa comments zoote ni muke ya muzungu alikuita mlala hoi aone sasa, muke ya muzungu atakuheshimu sasa, yani ni kama vile alifungua duka kwa ajili yangu mimi. Imagine hata baada ya hapo nilijikaza sikutaka kutoa hii infomation, ou know why? i though to myself, God has blessed me so much more than her and i know deep down she doesnt hate me but rather she wishes to have what i have kwanini nisimwache aenjoy this moment? kumbuka hapo just a weeka before yeye hakutaga hata nii enjoy mashauzi yangu ya kuwadanganyia ile mingazi kumbe nimeenda kwa jirani kwenye lobby ya watu woooote nkajifanya kwangu. Akaniumbua fasterrrrrrrrrrr.LOLEST.....

Maskini ya Mungu mimi i was sooo happy for her nikasema Mungu sitomwaribia huyu mwanamke swagga zake amestruggle sana kutafuta status mujini, kapitia mengi mnoooo ili aonekane na yeye yupo juu,nikasema her dream has come true, although alikuwa ananibeza anasema yeye haishi kwa mkopo..... Na pia mkopo sio kitu kibaya at all. Mkopo ndo sababu kubwa ya watu wa nchi zilizoendelea kuweza kuishi maisha mazuri. Ningekuwa mtu mbaya mimi ningejitumia hata comments za kuwataarifu kachukua mkopo tu huyo na msingejua comment nimetuma mimi ila sikutuma hata comment sababu i wanted her to enjoy her moment. Kweli unaweza kuniita mimi mtu mwenye wivu ? Choko choko zoooote alizonifanyia SInta and still niliamua kumstiri kama mwanamke mwenzangu ili aipate ile heshima aliyokuwa anaitafuta muda mrefu.  Alivyokuwa avyoshangalia furaha yake na kuringishia watu bado comments zote ni za kunishushua mimi tu na bado nilijikaza.

Sintah akaona mbona huyu Mange hatikisiki ?akaona atoke na style ingine,ndo jana akaamua kuweka comment ya BEDUI ya kumnanga mwanangu. (Najua ni comment ya Bedui coz aliituma kwangu  kwanza sikuiweka and i know her IPs)Hapa ndo niliposema ok now im justified.Chief, ukishatukana mtoto wa mtu all bets are off. Bedui kama nikiachia comments za kumtukana mwanae ni sawa tu maana BEDUI alikuwa anatukana wanangu facebook tena kwa jina lake bila woga. Pale waliponitajia Bhoke wangu bila haya wala huruma ndo nikasema ngoja nijiachie.

Sasa leo anaweka comments sijui anaziandika mwenyewe au vipi eti Sintah mlilie Mungu, Mange anajifanya tajiri wadunia, Mungu atamlipa. Nyie wajinga sikilizieni. Kama huyo Mungu wenu ndo Mungu yule yule aliemuumba mwanangu basi dua zenu hazinipati ng'oooo. Mumtukane malaika alafu mama yake awajibu then ndo mkumbuke kumlilia Mungu wajinga wakubwa.  Nyie mtaadhibiwa kwanza then ndo ntaadhibiwa mimi.

Sasa kwa wale mnaojifnaya mnajua sana kunikosoa na kunisema je ingekuwa ni wewe Sintah kakufanyia hivi, je  usingefanya nilichofanya mimi? MNIKOMEEEEEEEEEE NA MUMKOMEEEE BLACK BEAUTY WANGU..... Sinta nakurudia tena kwa vile mtoto wako anahitaji privacy zaidi ya watoto wa Klyn so huwezi kumwonyesha kwenye internet angalau tembea nae, angalau nenda nae kwenye birthday party na wewe uonekane mama.Kama yupo Uganda kamfate uende nae Dar ukae nae hata holiday tu uwe a proud mother even for a day. UKIWEZA KUFANYA HILO IM SURE UTAUJUA UCHUNGU WA MWANA NA UTAACHA KUNITUKANIA MWANANGU. MAANA A FEW MONTHS AGO ULIDIRIKI KUMTUKANA KWENYE POST YAKO. Naelewa kwa nini hujui ubaya wa kumtukania mtu mtoto ni kwa sababu wewe una moyo mkavuu wa kuweza kuishi maisha huku ukimficha kiumbe wako, kiumbe uliembeba mienzi tisa na kumzaa kwa uchungu. Im sure hata kama nikiamua kutumua data za yule dada alizonitumia siku zile kuhusu mtoto wako nikamchambua mtoto wako im sure hutoumia at all, yani sidhani hata kama utaajali maana hutaki hata kuwa mama yake, im sure ungeweza kumgawa ungemgawa fasta. Hata kama baba wa mtoto wako akijulikana itakuchafua sana still sio sababu ya kumchukia mtoto wako. YES, WAMESHANITUMIA MPAKA DETAILS ZA BABY DADDY WAKO ILA NITAKUSTIRI SABABU WEWE NI MWANAMKE KAMA MIMI SINA HAJA YA KUKUAIBISHA AU KUMUAIBISHA MTOTO WAKO. ILA BE CAREFUL SINTAH CHUNGA HILO DOMO LITAKUPONZA........USITAKE KUREKEBISHA TABIA ZA WATU WAKATI WEWE YAKO NDO INAHITAJI MAREKEBISHO KWANZA.

IM DONE NA CHAPTER YA KUKUPA USHAURI. SOMA VIZURI SIJAKUTUSI WALA KUKUDHARAU KAMA NILIVYOFANYA LAST TIME, ILA NIMEKWAMBIA UKWELI UKIPENDA UFANYIE KAZI USIPOPENDA UPOTEZEE.... SASA NAINGIA KWENYE KIPENGELE MUHIMU SANA.....MWENYE MACHO NA AYAONE....

Unajua mara nyingi binadamu tunakuwa hatumalizi matatizo yetu sababu tunakuwa na haraka  ya kudeal na tatizo bila kuangalia chanzo cha hili tatizo ni nini. Huyu SInta akiulizwa na mtu kwanini unamchukia Mange sidhani kama atakuwa na jibu la msingi. kwa kweli sidhani.Sasa jiulize kwanini SInta amekuwa Adui yangu mkubwa? ngoja niwapeni mambo ya mujini leo.Swaumu haikatazi kuongea ukweli inakataka kuwa mshari though.

Mnakumbuka that first trip nimerudi Bongo for the 1st time, kutua bongo tu kesho yake naamshwa naambiwa sinta kaweka macooment huko ya ugomviii. Nikashangaa huyu ananini? ofcourse ndo siku zile hakuna mtu anajua blog yake so akawa anaindika kwa chati ili watu wakasome. Sikumchelewesha nikimpigia simu shamim Mwasha sababu nilijua anaurafiki na SIntah nikamwabia naomba number ya Sinta, akanipa nikaruka hewani fasterrr, Nilimfurumushia Sinta matusi kama yake ya Wema kwenye ile video, ila nilikuwa nna hasira sana so full kigugumizi sidhani hata kama alikuwa ananielewa, yani angenirekodi siku ile kama Diamond alivyomrekodi Wema akanirusha mngecheka mpaka mlie machozi....lol...Sintah akawa mpoleee akanijibu kweli kuna comments sijaona ngoja nazitoa Mange, na ukweli akazitoa in 5 mins. Na kesho yake akaamka akawashushua msinigombanishe na Mange tumejuana toka enzi za polisi wanavaa kaptura...hahahahahahhahaha... Alfu ni kweli nimemjua Sinta toka nipo Chuo first year aliwahi hata kuja kunitembelea mabibo hostel.

Basi yakaisha maisha yakaendelea akaacha kunifatilia issue zangu. But after about a week tu ndo akaibuka na matusi ya kunitukana mara 10 ya before, yani kama alikuwa kapagawa na kitu, akawa kama vile adui yangu. Nikaa kimya coz nilikuwa nisharudi US. Then 2 months later nikarudi Bongo.The day nimeingia Bongo naamka tu Sintah akaweka yale maeil ya mimi kumcheat mume wangu. Nikamtwangia Shamim tena nikamwmabia Shamim mwambie Sintah hata anitafute vipi siwezi kumwandika kwenye blog au kumjibu sababu she is not my class yani mimi kugombana na SIntah ni kama Beyonce agombane na Cassy wa Pddy atakuwa kajishusha mnooo. SO atajijua, Shamim akacheka alafu nikamwmabia yani last time nilimtukana akaogopa akatoa akajifanya msinigombanishe na Mange, Shamim akastuka akaniuliza ulimtukana? nikasema ndio?akasema wewe mwenzio kaniambia ulimpigia ukamwambia unaomba atoe hutaki mgombane, ukamwomba msameheane, ndo akakuonea huruma,. Nikachekaaaa nikamwambia uwiiiii kawadanganyajeee nani amwombe yule? hana hadhi hiyo.Kesho yake nikamuuliza hivi Sinta anafnaya wapi kazi akanijibu anasemaga yeye ni secretary wa Manji ila sijui ofisi zao. nikasema poa.maana mpaka hapo nilikuwa nimesema haya mambo ya internt ya kitoto ngoja nikamfate face to face tumalizane. Still nikawa na avoid kurespond kwenye blog maana ingekuwa kubwaa balaa so nikampigia tena Shamim, Shamim akanijibuje aah mie siongei na Sinta bwana nimechoka, ila Mange unajua kwamba wewe ndo ulianzisha hii style ya kutukana watu kwenye blg? Sinta anakuiga tu ila wewe mwneywe ndo ulianzisha. Nikamwmabia Shamim sikatai mie ndo nilianzisha hiyo ila mind you naandika mtu alieniletea shobo sio mtu ambae simjui hanijui. Mtu mzima akikutana sio lazma akwambie shenzi, nikaelewa pale pale Shamim anachosema ni kwamba i deserve yale matusi Sintaha aliyotukana  sababu mie ndo nimemfundisha Sintah hapo mambo.Baada ya kupata jibu la shamim nikajua kimenuka tayari, mpare kama mnavyonijua sio zoba nikajumlisha moja na mbili, nikamtwangia mtu huyo mtu alikuwa anajua story yoooote kwa kuhadisia na Sinta yeye ndo akanipa mkanda mzima.

Sasa this is what happened....... Mnakumbuka nimesema first time nilimpigia Sintah nikamtukanaaaaaaa matusi ya nguoni akaogopa akatoka comments na kesho yake akawashushua mukome kutugombanisha???  To be fair alivyoandika ile SInta alimaanisha na alijiskia vibaya na tuka move on na maisha. Sasa guess what changed things? Si mimi nilimwambia shamim kuwa nilimtukana Sinta atoe makoment akaogopa? Shamim akamtwangia Sinta, shoga mbona ulisema Mange alikuomba msamaha kaniambia alikutukanaaaaaaaaaaa, ukawa mdogo kama piriton, anasema ulitetemekaaaa yani alikukomesha. Sasa kama mnavyojua kila binadamu kaumbwa na pride na yeye Sintah akaona kwanini nimejigamba? Ndo sasa ikabidi amuonyeshe Shamim na wapambe wengine kuwa haniogopi. Shamim akamwambia kuwa nimesema  mimi ni beyonce siwezi kugombana nae, Imagine sikusema mimi Beyonce nilimdharau ofcourse ila maneno yalirembwa zaidi. Akamwambia pia kuwa nilikuwa namuulizia anapofanya kazi au anaopishi, so huko JLO TZ akapandisha mzuka balaaaa ndo akazidisha mara elfu nane kunisengenya. Ila mie nilijiuliza hivi what has changed since Sinta kuniomba Mange natoa na kuweka ile article kuwaaambia Najuana na Mange long time na ghalfa kubadilika vile nilijua lazma kuna kitu but nilikaa kimya.

So as much as yule Sinta ni mtafuta shari muda wote ila mwisho wa siku ugomvi wangu wooooooooooote ule na JLO usingetokea kama sio Shamim Mwasha. Shamim ndo aliepanda mbegu na mzizi wa fitna. Kwa wale mliokuwa mnanisema kuwa mimi ni m mbaya kwa nini niachie comments za kumtukana mume wa Shamim na maswali mengine kibao. Naombeni mkae mkijua kuwa mimi sio kichaaa siwezi eti kuanza kumtukana mtu eti sababu harusi nzuri eti nna wivu. Chief sina wivu na pesa ya sembe.....lol... Ila kwa kweli niliona kwamba nimetukaniwa wazazi wangu,ndugu zangu,biashara yangu, wanangu, mimi mwenyewe, na Sinta katukaniwa mama yake, mtoto wake na yeye mwenyewe wakati aliesababisha katulia pembeni anajifanya dada wa heshima. Nikaona bora na yeye atukanwe ajue utamu wake. Alafu akiulizwa na watu huko bongo kwanini Mange anakufanyia hivi? anajibu si mnamjua Mange ana matatizo yani sijui nilichomkosea itakuwa ni sababu Sintah alivyomchamba alinitaja jina langu na nilimwambia Sinta atoe jina langu wasinihusishe Sinta hakutoa nilichukia sana.

Sasa ndo mjue hawa wadada mnaowaona wana heshima zao hawagombani na watu blog zao hazina matusi mkadhani wanafanana na blog zao. Ni mafisadi na mahasidi , wanafki , waswahili , wapenda ugomvi kushinda Mange na Sinta. Bora Mange Kimambi nawaonyesha tabia zangu  ubaya wangu na uzuri wangu kuliko hawa wanaokaa kujidai ni wenye heshima kwenye jamii kumbe kasheshe zote zinazotokea kwenye jamii ni kazi yao.

Shamim mimi sipendi unafki kama ulikuwa hunipendi ulikuwa unanichekea ya kazi gani? nILIKUWa nakupa wewe malalamiko ya Sinta sababu na mimi nilidanganyika kama jamii yote nikawa nkuona mtu mwenye hekima nikasema ngoja Shamim ayamalize chini kwa chini kuliko na mimi kwenda kwenye blog kumjibu Sinta nikanufaisha watu, Kumbe nilikuwa nimeingia choo cha kiume bwana, badala ya kusuluhisha anatengeneza balaaa. Wewe mtu umeshaona kwamba Sinta kaweka post kwamba sina tabu na Mange kwanini usifurahii ukaayacha, hata kama Sinta alikuwambia Mange alinilamba miguu ndo nikaona nitoe macomment na mimi nikamwambia she lied  ulikuwa na haja gani kwenda kumtia Sinta moto kumwambia Unamwogopa Mange Kasema amekutukana mpaka ukatia akili? hukujua kama Sinta kama binadamu lazma na yeye angetaka kuwaonyesha nyie kuwa haniogopi? Ulijua sana.

dada wa kistaarabu uliemfano wa kuigwa na wanawake wengine. Kwa vile unataka kuonekana decent mbele za watu huku unachonganisha watu alafu unakaa pembeni ngoja niwafahamishe who you really are. Although umeweza kujipenyeza penyenza kwa nguvu mpaka ukaingia kwenye cirlce ya wadada wa mujini  aisee wewe bado ni mwanamke wa uswahili hutokaa kuacha asili. Ndo maana ni mnafki.

Wewe mwanamke decent mwenye blog ya heshima umeolewa ndoa ya funika bovuuuuuuuuuuuu umewaeleza wanawake wenzio mume umemtoa wapi? Mambo ya wenzenu mnapenda kuyaweka wazi ya kwenu kimyaaaaa kisa muenekane hamna drama. Naomba ueleze kadamnasi kwanini  Mbonie Masimba who was your best friend, wa pika na kupakua hakushiriki wedding yako wakati alikuwa hapo hapo Bongo? Umewaeleza kuwa  Huyu "businessman" wako alikuwa ni bwana wa Mbonie ukamwibia mwezio na kuua urafiki.,hata kama Mboni hakuwa mke ila ulijua kama ni mtu wa Mbonie,  umeemuumiza sana sana sana mwenzio. You will never admit ulichomfanyia Mbonie sababu wewe ni 'decent' Kutwa kunisema mimi mgomvi , mimi nna matatizo chief ILA pamoja na maugomvi yangu yoooooooooooote im sure hujawahi kusikia nimemfanyia mtu unyama ulioufanya wewe kwa Mboni. Yani wewe huo umgovi mmoja ni umefunika miugomvi yangu yooote.

Alafu  ooooh  women's day, wnanawake tupendane, tupongezane, wewe mwenyewe umeshindwa kumpenda shosti wako Mboni ukamwimbia bwana wake hukujali urafiki ili mradi upate mume mwenye pesa ndefu utingishe mji alafu unawaambia wenzio tupendane womne's day. Ingawa ulijaribu sana kuficha kila mtu anajua how close you were with Mboni na Mboni anajulikana ni mpenda mashughuli , sijui kama kuna harusi Mboni hajaenda mji huo, hata yangu alikuja maskini akachangamsha , hana wivu na mtu ukiolewa anakupa full support. Leo hii mboni hakuonekana kwenye shamra shamra za harusi unadhani ingebaki siri? Mdada wa watu mkampeleka invitation siku ya harusi...lol

Mboni usiumie mpenzi, malipo duniani, Karma is a bitch. Kwa sasa hivi jamii inakuheshimu wewe kuliko yeye, hata kama huna maisha kama yake ila unajituma na pesa yako ni ya halali,usiumizwe roho wala usirushwe roho na mashauzi ya pesa zilizozajaa damu za vijaa wa Kitanzania na machozi ya kina mama wa kitanzania wanaowaliliwa watoto wao waliokuwa mateja.

Ulivyokuwa huna kitu hakuna aliekujali mjini kama huyo mbonie wengine wote walikuwa wanakualika for pictures basi. Umepata visenti wanakukenuliwa unawasahau waliokupenda enzi zile....Lol...

Narudi kwako Sinta, umejitafutia mabalaa kibao kwa kusikiliza maneno ya kupampiwa , haya sasa ulivyomtaja jina lake siku ile alikununiajeeee???? sasa huyo ni rafiki? angekuwa anakupenda ange stand with you, ila hakutaka kujihusisha na wewe.Shamim unachonganisha watu alafu ukitajwa hadharani kama mpeleka maneno unajifanya kumind ili tu umentain status yako ya u'decent'.  Sinta penda unapopendwa na wewe usijipendekeze sababu sijui umepewa duka bure, unajua mwenyewe, Unaendaga Sea clif kula mwenyewe kwenye meza kama mchawi unaweka picha kwenye blog mbona usiende na dadako Shamim? Birthday walialikwa wenye class mwenzangu na mie hukupata mwanaliko sababu huna hadhi ya kukaa meza moja na wadada wa mujini, alafu bado unagombana na watu ili umuonyeshe Shamim we gangwe?

Kama ulikuwa hujui, Dar hupati marafiki kama huna kitu. Umeona mwenzio alivyopata marafiki wa kona zote sasa hivi eeeh? sasa hata ujipendekeze vipi kwake, hata ufanye nini huwezi kupaka mialiko ya juu sababu wanakuona huna kitu.

Ila usingetafuta maneno na watu wasingejua umepataje pataje hata duka la Wedding dresses , naamini ungepata angalau shoga wa kwenda nae out. Ila ndo hivyo tena umeharibu mwenyewe. Mwenzio hapa hata nigombane vipi na watu siwezi kukosa wa kula nae bata bongo....

sasa wewe mwenzangu na mie umejiingiza kwenye maisha ya kutafuta shari, mji mzima wamekuchukukia alafu ukiongeza juu ya hapo wanakuona huna kitu, chief utatembea peke yako mpaka basi, na mume ukimpata itakuwa bahati sana. usigeze ubabe wangu mwenzio nimejikamilisha.......shauri zako.....

Na kama  unataka kufanya mashauzi uwaogopeshe kidogo mimi sina roho mbaya ya kutaka kutaka kukuumbua, ila sasa ukitaka kufanya mashauzi huku unanichokoza ndo hivi utakuwa unajiharibia.

SINA KINYONGO NA WEWE SINTA,NAJUA HAIKUWA AKILI YAKO ULIKUWA UNATAFUTA DUKA LA BIASHARA. I CAN RESPECT THAT. ISHI KWA AMANI.....

Nimemaliza jamani, sasa muache kuwasifu wadada wa mji huu sababu tu eti hawatukani wapo kimya mkiwajua mambo yao mtaona bora kina Mange.......

Wadada wa mujini na nyie kwa kupenda watu wenye pesa na kupapatikia harusi zisizo na michango, yangu ilikuwa na haki ya kupapatikiwa kwa kutochangisha sababu mume wangu anajulikana anafanya nini, ila nyie mnachetukaaaaaaaaaaaaaa na kupagawa na harusi ambazo hamjui pesa zimetoka wapi. Kuna siku mtajakuta mihela mliochetuka nayo ndo iliyosababisha ndugu yako kawa teja.... Mlikuwa mnamnyali before, sasa hivi mmemuona class yenu....lol.....

Shikamooni wakubwa, MSIJISTRESS KUSOMA HILI GAZETI PAPO KWA PAPO, TUMIA HATA SIKU MBILI MSIJE FUKUZWA KAZI MAKAZINI HUKO....

PS Narudia tena staki comments kijinga na matusi kama una comment naoimba uwe ya kiutu uzima,. Everyone is welcome to comment except you Bedui.Please take a break today, maana najua hii topic itakupandisha BP." Mange


Source:Mange website

About Syed Faizan Ali

Faizan is a 17 year old young guy who is blessed with the art of Blogging,He love to Blog day in and day out,He is a Website Designer and a Certified Graphics Designer.

0 comments:

Post a Comment