Thursday 11 July 2013

HUYU NDIYE MWANAMKE "KIJEBA" ALIYEKWAMA KUKUA KWA MIAKA 15 SASA, AVAA NGUO ZA WATOTO..


By on 06:20

KUSHOTO: Laxmi akiwa na mdogo wake, Suman. KULIA: Laxmi akijaribu kuvaa viatu vya watu wazima.
Amekuwa akishuhudia rafiki zake wakikua kufikia kuwa wasichana wakubwa lakini Yadev Laxmi hajabadilika tangu alipokuwa na umri wa miaka mitano.
Anaweza kuwa na miaka 20 lakini bado ana urefu wa futi 3 na inchi 3 tu, huku akiwa na uzito wa kilo 3 tu na kuvaa nguo za watoto wa miaka sita.
Mvurugiko adimu wa kinasaba umesababisha Laxmi kukoma kukua miaka 15 iliyopita na amestaafu kuishi kwa maisha yake yaliyobaki kama mwanamke aliyenaswa katika mwili wa utoto.
Laxmi amepitia miaka kadhaa ya kuonewa na kudhihakiwa lakini anasema jambo gumu zaidi kukabiliana nalo ni hatima yake iliyokataliwa na hali yake.
Anafahamu hawezi kamwe kuja kuwa na watoto na hivyo haoni sababu yoyote ya kuolewa.

Anakiri amekuwa pia akitishwa na kumwamini mwanaume na hofu ya kudharauriwa katika ndoa.
Laxmi, anayetokea Gurgoan, nje ya New Delhi, alisema: "Wakati mwingine nafikiri kuhusu maisha ya kawaida ambayo ningeweza kuwa nayo na inanifanya nijisikie mnyonge.
"Ningeweza kuwa na furaha na uhuru na kufurahia maisha waliyonayo wasichana wengine."
Miaka ya dhihaka na hofu kuhusu kutekwa nyara yamemuacha Laxmi akiwa na mashaka makubwa kutoka nje peke yake lakini anasema anamudu kuendana na mapungufu yake hayo kupitia msaada kutoka kwa familia yake.
Mama yake, Parvati, mwenye miaka 52, anamnunulia nguo kumsaidia kuepuka manyanyaso ya kununulia nguo kwenye sehemu ya watoto.
Kaka yake Azad anasumbuliwa na hali kama hiyo lakini akaendelea kushikilia taaluma yake kama mwalimu na anaamini manyanyaso yamemfanya kujitahidi zaidi kufikia malengo yake.
Mdogo wake wa kike Suman, mwenye miaka 15, ambaye ana kimo cha kawaida, humchunga Laxmi nje na humsaidia 'kumhamasisha'.
Laxmi anasema: "Sipendi kukutana na watu wapya kutokana na kunichoma wanaponishangaa na kunionea kila wakati."
Lakini anasema kwa kufuata uongozi wa Azad na kwa msaada wa baba yake Bahadur na mama yake, anakabiliana na hofu zake na kuanza kazi kwenye duka moja.
Laxmi anasema: "Ninahofia lakini niko imara na nitazishinda hofu zangu zote kwa kufanya hivi."
Fedha hizo zitakuwa muhimu kwa familia yake, ambayo inategemea Rupia 8,000 (Pauni za Uingereza 88) kwa mwezi ambazo baba yake anapata kutokana na kazi ya ulinzi.
Kipato kidogo cha familia hiyo tayari kimeanza kuandamwa na mfululizo wa majanga.
Hawawezi kumudu fedha zinazohitajika kugharimia homoni za kukuza binadamu kwa ajili ya Laxmi na Azad.
Hali zao zingeweza kuimarika kama wangeweza kupatiwa kabla ya kufikisha umri wa miaka 16 au 17.
Madaktari wanasema baadhi ya matibabu yanaendelea kuweza kupatikana lakini yanaweza tu kufanikiwa kama yatafanyika mapema.
Hatahivyo, licha ya magumu yake, Laxmi amestawi kwenye maomo yake.
Amehitimu sekondari ya juu kwa kupata alama za juu kabisa na sasa anataka kuanza kozi ya kompyuta kwenye chuo kimoja.

About Syed Faizan Ali

Faizan is a 17 year old young guy who is blessed with the art of Blogging,He love to Blog day in and day out,He is a Website Designer and a Certified Graphics Designer.

0 comments:

Post a Comment