Wednesday, 17 July 2013

M2 THE P ASHINDWA KUONGEA YALIYOWAPATA MPAKA NGWEAR AKAFARIKI AISHIA KUSEMA HAYA


By on 22:19

Kwa mara ya kwanza toka kitokee kifo cha rapper Albert Mangweha (Ngwair) rafiki yake wa karibu ambae ni M2TheP waliekua pamoja Afrika Kusini mpaka umauti umemkuta Ngwair, amefanya interview kwa mara ya kwanza kwenye radio kupitia XXL ya @CloudsFM na kuzungumza machache pamoja na kutambulisha single yake mpya na ya kwanza toka kifo kitokee.
M alishindwa kujibu maswali mengi yaliyotaka kujua kilichotokea kwa Ngwair na akaishia tu kukanusha kuhusu ishu za dawa za kulevya kwa kusema sio kweli kwa sababu siku zote dawa za kulevya huwa hazichukuliwi South zikaletwa Tanzania bali huchukuliwa Tanzania na kupelekwa South Afrika.
Akiwa bado anajisikia uchungu kwa kile kilichotokea kwa Ngwea, M2theP alishindwa kueleza kuanzia mwanzo mpaka mwisho lakini akaahidi kukisema chote siku chache zijazo mbele ya Waandishi wa habari.

About Syed Faizan Ali

Faizan is a 17 year old young guy who is blessed with the art of Blogging,He love to Blog day in and day out,He is a Website Designer and a Certified Graphics Designer.

0 comments:

Post a Comment