Mapendekezo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wanachama na viongozi wake.
UTANGULIZI
1.1
Mnamo tarehe 03/06/2013 Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitangaza rasimu
ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1.2 Rasimu hii ya Katiba itajadiliwa katika mfumo wa aina mbili wa mabaraza:
Mabaraza ya Katiba ya Wilaya,
ambayo yameshaundwa na yatatoa maoni yake kupitia mikutano
itakayoitishwa na Tume ya Marekebisho ya Katiba. Mabaraza haya
yanasimamiwa na Tume yenyewe.
Mabaraza ya Asasi,
Taasisi na makundi ya watu wenye malengo yanayofanana kama vile vyama
vya siasa na jumuiya za kidini na kadhalika. Mabaraza haya yanasimamiwa
na Asasi au Taasisi husika.
1.3 Chama Cha Mapinduzi kimeshajiunda
kama Baraza la Katiba la kitaasisi na kutambuliwa rasmi na Tume kwa
barua Kumb.na. AB 76/386/57 ya tarehe 24/052013
1.4 Kwa
kuzingatia kwamba Chama Cha Mapinduzi ni Taasisi muhimu na yenye
masilahi makubwa katika upatikanaji wa Katiba Mpya, Kamati Kuu ya
Halmashauri ya Taifa iliyokutana mjini Dodoma Tarehe, 10/6/2013, pamoja
na mambo mengine ilielekeza kwamba uandaliwe utaratibu utakaohusisha
utoaji wa maoni utakaotumiwa na wanaCCM kutoa maoni yao.
1.5
Madhumuni ya ufafanuzi huu ni kujenga uelewa wa pamoja wa maudhui ya
Rasimu ya Kwanza na hivyo kuwawezesha wanaCCM kushiriki kutoa maoni yao
kikamilifu kutoka ngazi ya matawi hadi taifa.
UTARATIBU WA KUTOA MAONI
2.1 Kwa upande wa matawi maoni yatatolewa kupitia mikutano
Kwa wilaya, mikoa na taifa. Maoni yatatolewa kupita halmashauri kuu zao.
2.2
Ili kupata mfumo wa aina moja wa kuijadili Rasimu ya kwanza na kutoa
maoni, wanachama wanaelekezwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:
-->Kuitaja sura ya Rasimu ya Katiba inayohusika
-->Kutaja ibara ya Rasimu ya Katiba
-->Kutoa maelezo juu ya Ibara hiyo (kama kuna upungufu au maoni mengine yoyote);
-->Mapendekezo ya marekebisho
-->Sababu za mapendekezo ya marekebisho hayo.
0 comments:
Post a Comment