Saturday, 20 July 2013

MSHIRIKI WA TANZANIA "NANDO" KUPANINDISHWA KIZIMBANI BAADA YA KUMZALILISHA "SELLY" KWA MADAI AMEMWAMBUKIZA GONJWA LA ZINAA NDANI YA JUMBA LA BIGBROTHER


By on 13:30


Mshiriki wa pekee katika Jumba la BBA The Chase Selly kutoka nchini Ghana, amesema ya kwamba yupo mbioni kumfungulia mashtaka mshiriki kutoka nchini Tanzania Nando kwa kitendo cha kumdhalilisha na kumsingizia amemuambukiza Ugonjwa wa Zinaa.

Baada ya kutolewa katika jumba hilo wiki iliyopita, Selly ameshauriwa na mama yake na tayari wamewasiliana na Waandaji wa Shindano hilo. " Nimepima  sijakutwa na maambukizi ya aina yoyote ya Magonjwa ya Zinaa wala sina historia hiyo" Alisema Selly.

" Mimi na Nando hatukufanya Mapenzi zaidi ya kucheza tu Kitandani, nashangaa hata kwa kiasi gani mambo yamekuwa hivi" Aliongeza Mrembo huyo.

About Syed Faizan Ali

Faizan is a 17 year old young guy who is blessed with the art of Blogging,He love to Blog day in and day out,He is a Website Designer and a Certified Graphics Designer.

0 comments:

Post a Comment