Miili ya wanajeshi saba mashujaa wa Tanzania waliofariki wakiwa kazini
wakitekeleza ulinzi wa amani wa kimataifa katika mkoa wa Darfur nchini
Sudan, imewasili leo kwa ndege maalumu ya Umoja wa Mataifa.
Kaimu
Mkurugenzi wa habari wa JWTZ, Meja Joseph Masanja amesema miili hiyo
imewasili leo Jumamosi majira ya saa 9.45 alasiri katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa JNIA na imehifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya
Lugalo hadi Julai 22 ambapo itaagwa rasmi.
Miili iliyowasili ni
ya Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma,
Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney Ndunguru, Pte. Peter Werema na Pte.
Fortunatus Msofe.
Shughuli za kuagwa miili ya wanajeshi hao
zitafanyika katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga
taifa vilivyoko Upanga jijini Dar es salaam.
Kuwapoteza wanajeshi
hawa ni la kwanza na kubwa kwa nchi ya Tanzania tangu Tanzania
ilipoanza kuchangia walinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka
2007. Wanajeshi wengine watatu wa Tanzania walifariki dunia mwezi
uliopita baada ya chombo chao cha kusafiria kusombwa na maji ya mto
uliokuwa umefurika huko nchini Sudan.
0 comments:
Post a Comment