Saturday 27 July 2013

‘RAMA MLA WATU’ APELEKWA MIREMBE KWA UKICHAA


By on 11:46

 Ramadhan Seleman ‘Rama Mla watu’, aliyekuwa akishikiliwa na dola kwa tuhuma za mauaji ya mtoto, Salome Yohana licha ya kuondolewa hatia hiyo huku akiwekwa chini ya uangalizi baada ya kubainika kuwa na matatizo ya akili, Jumatano iliyopita alirudishwa hospitali ya waalifu ya Isanga iliyopo Mirembe, Mkoani Dodoma. 
Rama alipandishwa basi ya Shukrani majira ya saa moja asubuhi akiwa na askari wawili waliokuwa wakimlinda kuhakikisha wanamfikisha kwenye hospitali hiyo, mpaka akili yake itakapotengemaa ndipo ataachiwa uraiani.
Kijana huyo alisafirishwa kupelekwa hospitalini huko kufuatia amri iliyotolewa na Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam katika kesi yake ya mauaji iliyokuwa ikiwakabili na mama yake, Khadija Musa, baada ya kubainika kuwa alitenda kosa hilo akiwa na matatizo ya akili.

About Syed Faizan Ali

Faizan is a 17 year old young guy who is blessed with the art of Blogging,He love to Blog day in and day out,He is a Website Designer and a Certified Graphics Designer.

0 comments:

Post a Comment