SIRI nje! Lile skendo la Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’, kudaiwa kulala na mwigizaji Irene Uwoya ambaye ni
mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ limevuja.
Huku akijua kabisa kuwa ataibua zogo kwa kuwa Uwoya ni
mke wa ndoa wa mtu, kwa mara ya kwanza, Diamond ameamua kuanika kisa
kilichomfanya kujiweka kwa muda kwa Uwoya.
Kwa mujibu wa chanzo cha
kuaminika cha gazeti hili, kilichomfanya Diamond kufikia hatua ya
kumtongoza na kutoka naye kimapenzi, ni kitendo cha Uwoya kutoa maneno
ya kumponda huku akionesha waziwazi hali ya kumchukia kila walipokutana.
UWOYA ALIKUWA HAMPENDI DIAMOND
“Unajua
Irene (Uwoya) alikuwa hampendi Diamond hata siku moja na mara nyingi
alikuwa kila akimuona lazima amponde. Habari hizo zilikuwa zikimfikia
mwanamuziki huyo kupitia mashoga wa mwigizaji huyo ambazo ndiyo
zilichochea.
“Kufuatia hali hiyo, Diamond naye kila alipofikishiwa
taarifa na mashosti wa Uwoya, alikuwa akijisikia vibaya mno ndiyo maana
‘Sukari ya Warembo’ alilazimika kumvizia Uwoya kwa hali na mali ili
kumfanya ampende.
CHIKOKA ATAJWA
“Nakumbuka kwa mara ya kwanza Diamond alimtuma (Juma) Chikoka ‘Chopa’ kwa Uwoya ili amfikishie ujumbe wa yeye kumtaka.
“Chikoka
hakufikisha taarifa hizo, kitendo ambacho kilimuuma sana lakini siku
moja Diamond alikutana na Uwoya akiwa na Chikoka, maeneo ya Sinza-Mori
(Dar), akamuomba tena Chikoka namba, akampa, hapo ndipo uhusiano
ulipoanzia.
“Siku mbili baadaye Diamond alizungumza vizuri na Uwoya.
“Diamond
aliomba ahadi ya kukutana na mwigizaji huyo, bila kuchelewa, Uwoya
aliiva na kukubali ambapo walikutana kwenye ile hoteli kule Mbezi Beach (Dar) wakamalizana.
“Unajua Diamond alifanya hivyo kwa sababu ya kupondwa na washikaji zake kuwa anatamba kutembea na mastaa lakini hamuwezi Uwoya.
“Kwa
hiyo utagundua chanzo cha yote ni mdomo wa Uwoya kutangaza kutompenda
Diamond kwani alikuwa akimsema vibaya sana kwa watu wake wa karibu,”
kilidai chanzo chetu.KUMSIKIA DIAMOND
Baada ya
kujazwa habari hizo, mwanahabari wetu alilazimika kumtafuta Diamond ili
kuhakikisha kama alichoelezwa kina ukweli ndani yake ambapo bila
kinyongo, mkali huyo wa wimbo wa Kesho alifunguka:
“Dah! Japo yalishapita ila ni kweli Uwoya nilikuwaga nikipata taarifa kutoka kwa marafiki zangu kuwa alikuwa ananichukia sana.
“Nilikuwa
nikijiuliza sababu za yeye kunichukia lakini nikawa sizipati hata
kidogo na hata nilipochunguza niligundua kweli alikuwa hanipendi kabisa.
“Sipendi
sana kuzungumzia ishu hiyo ila naweza kukubali kweli kuwa marafiki zake
na wangu ndiyo walionichochea sana kukutana na Uwoya na sasa hatuna
tatizo na tunaishi kwa amani na upendo ingawa mengi yamepita na
yaliyosemwa sina sababu ya kuyashikilia, kikubwa tumuombe Mungu.”
KAMA KAWA UWOYA HAPOKEI SIMU
Ili
kupata mzani wa habari hiyo,tulimwendea hewani Uwoya
lakini kama kawaida, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE
Miezi
kadhaa iliyopita,iliripoti
habari ya Uwoya na Diamond kunaswa usiku katika moja ya vyumba vya
hoteli maarufu kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi huko Mbezi Beach, Dar
ambapo habari hiyo iliibua maneno lakini sasa mwanamuziki huyo amemaliza
utata kwani nguzo na sifa kuu ya ni kuandika ukweli
siku zote.
0 comments:
Post a Comment