Wednesday, 10 July 2013

Tangu Jana Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Kamanda Alfred Lwakatare amelazwa hospitali ya Muhimbili(Pichani).Nanukuu maelezo yake hapa


By on 06:17

‘’Mkirejea tatizo la kiafya nililolipata nikiwa Central Police baada ya kukamatwa; la kuumwa sana na mgongo/mkono na baadaye nikiwa gerezani Segerea nilipelekwa Muhimbili Moi na baada ya vipimo (M.R.I) wakabaini kuna ulazima wa kufanyiwa upasuaji. Tatizo hili limeendelea na hata baada ya kutoka Segerea na nimekuwa nikiwaona madaktari kwa ukaribu. Jana mchana,imelazimu kulazwa hospitali ya Muhimbili ward ya Sewahaji NO.18,chumba No.024 kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Kama ilivyo kawaida yetu; Tunaanza na Mungu,Tunaendelea na Mungu na kumaliza na Mungu.
Tuzidi kuombeana na yote tumkabidhi Mungu.
Nawapenda sana!’’

Ofisi ya Katibu Mkuu imetuma timu kutoka makao makuu muda mfupi uliopita wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Katibu Mkuu Mzee Victor Kimesera ambayo ilienda kumjulia hali.
Kipindi chote alichoshikiliwa kwa makosa ya kubambikiza kimemletea athari kubwa sana kiafya.Ni jambo la ajabu sana tunafanya siasa za kishetani kubambikizia watu kesi bila kujali uhai wa mtu.

Tunaomba tuungane tena katika hili kama tulivyoungana katika kipindi chote cha kesi

About Syed Faizan Ali

Faizan is a 17 year old young guy who is blessed with the art of Blogging,He love to Blog day in and day out,He is a Website Designer and a Certified Graphics Designer.

0 comments:

Post a Comment