Jeshi la Polisi Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, linawashikiliwa watu wawili, wanaodaiwa kuwa ni mtu na mpenzi wake kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin kilo mbili zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi Sh90 milioni...Msichana inasemekana ni mfanyakazi wa shirika moja kubwa la ndege hapa Tanzania..
Mkuu wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa aliliambia
gazeti hili jana kuwa watuhumiwa hao ambao mmoja ni mwanamke
walikamatwa juzi saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA).
Alisema watuhumiwa walikuwa wakisafiri kwenda Mji
wa Bangkok Thailand kupitia Addis Ababa, Ethiopia ambapo walikata tiketi
ya ndege la shirika hilo.
“Walipoanza kufanya ukaguzi watuhumiwa hawa
walijichomeka katikati ya wenzao ndipo tulipowanasa na dawa hizo ambazo
walizificha kwenye mabegi yao katikati ya nguo,” alisema Nzowa.
Alisema kuwa watuhumiwa hao waligawana dawa hizo
kwani walipofanyiwa upekuzi na polisi walikutwa kila mtu akiwa na
kilo moja.
Source:Mwananchi
Source:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment