WINGU zito limetanda kwa askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),
katika nchi za Sudani Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Wakati Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya wanajeshi saba wa
jeshi hilo waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, Sudani kwa
kushambuliwa na waasi, nchini DRC yamezuka mapigano makali baina ya
waasi na majeshi ya Serikali.
Mapigano hayo yameripotiwa kuibuka kati ya Wanajeshi wa Serikali na
waasi karibu na mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC).
Msemaji wa wapiganaji wa waasi wa M23, ameliambia
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa ndege za kivita za
Serikali zimefanya mashambulio ya anga katika maeneo yao usiku wa
kuamkia jana.
Umoja wa mataifa kwa upande wake umesema uko tayari
kutumia nguvu, kuwalinda raia ikiwa wapiganaji hao wa M23 wataingia
katika mji wa Goma.
Raia wakimbia mapigano
Wakati huo
huo, mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu, yamesema kuwa zaidi ya
wakimbizi elfu sabini raia wa Congo wamekimbilia nchi jirani ya Uganda,
kukwepa mapigano hayo.
Wapiganaji wa waasi wa Uganda nchini
Congo, Allied Democratic Forces walishambulia mji wa Kamango na
kusababisha mapigano makali kati yao na jeshi la serikali.
0 comments:
Post a Comment