Friday, 19 July 2013

AIRTEL YAZIMA LAINI ZA SIMU ZISIZOSAJILIWA 200,000 ILI KUONGEZA USALAMA


By on 03:46

Dar es Salaam, Tanzania 18 Julai 2013, Airtel Tanzania
imetangaza itatimiza tamko la serikali la kuzima laini za
simu ambazo hazijasajiliwa ikiwa ni utekelezaji wa
sheria ya posta na mawasiliano ya kielektroniki ya
mwaka 2010 na muda wa hitimisho wa kusajili namba
uliowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
wa tarehe 10 Julai 2013
Usajili wa namba ni mchakato wa kuhakiki na kuweka
kumbukumbu za mtumiaji wa namba ya simu
unaowekwa na mtoa huduma za mawasiliano ya simu,
maelezo ya usajili ni pamoja na namba ya simu, tarehe
ya kuzaliwa, jinsia, sanduku la posta, namba nyingine ya
simu kama ipo, kitambulisho na namba ya kitambulisho
kilichowakilishwa
Akiongea kwa niaba ya Airtel, Mkurugenzi wa
Mawasiliano na Usimamizi wa Sheria Beatrice Singano
alisema" wateja wetu wote walijulishwa mapema kusajili
simu zao na tumetoa muda wa kutosha kwa zoezi hili la
usajili kufanyika ili kuepuka kufungiwa simu zao.
Tumetimiza sheria kama inavyosema ya EPOCA na
kufunga simu zote ambazo hazijasajiliwa
kuanzia usiku wa tarehe 10 julai kama mamlaka ya
mawasiliano ilivyowatangazia mwezi wa April mwaka
huu, kwa sasa jumla ya wateja wetu 200,000
tumewafungia mawasiliano kwa kutotimiza tamko hili la
kusajili namba zao za simu za Airtel
Tunaamini kwa kufungia simu hizi kuna wateja watabaki
bila mawasiliano hivyo tunachukua nafasi hii kuwaomba
wateja ambao hawajasajili simu zao kufanya hivyo katika
vituo vyetu vya huduma ikiwemo, maduka yetu ya Airtel,
wauzaji wa bidhaa zetu wa rejareja na mawakala wetu
wote nchi nzima. Pia kwa wateja wanaonunua namba
mpya kuanzia sasa wasajili namba zao ili waweze
kuzitumia. Pamoja na hilo pia tunawashauri wateja
waliosajiri kuhakiki usajili wao kwa kupiga*106#.
Tunaamini zoezi la
usajili litasaidia kudumisha Amani na usalama wa
watanzania na zaidi ya yote kukuza sekta ya
mawasiliano.
Usajili wa namba za simu umekuwa ukiendelea kwa
miaka michache katika ukanda wa jumuiya ya Afrika
mshariki (EAC) ikiwa na lengo la kudhibiti matukio
yanayofanyika kwa kutumia namba zisizosajiliwa
ikiwemo, wizi kwa njia ya mtandao, utekaji, ujumbe wa
matusi, ugaidi na mengine mengi
Kenya na Tanzania imepiga hatua na kufikia zoezi la
kuzima simu nchi nyingine za jumuiya ziko katika atua
ya awali za utekelezaji, Uganda iko katika hatua ya
utekelezaji wa usajili wa namba za simu.
Duniani kote mtumiaji wa simu anatakiwa kusajili simu
kadi yake mpaka pale itimisho linapotokea . na mteja
yoyote anayeshindwa kusajili simu yake mpaka muda wa
hitimisho simu yake itafungiwa na mteja atapoteza
namba yake, hivi karibuni usajili wa namba umeendelea
katika nchi za Ghana, Sierra Leone Nigeria, Zimbabwe,
South Africa, Kenya, Singapore,
Malaysia, Geneva, India, Egypt na nchi nyingine
Singano amewakumbusha mawakala na wasambazaji wa
Airtel kutimiza agizo hili na kuhakikisha kuwa simu kadi
yoyote inayouzwa au kupewa mteja iwe imesajiliwa
kabla ya matumizi, ni kosa la jinai kutumia simu kadi
isiyosajiliwa
"Mchakato huu ni wa lazima chini ya sheria ya posta na
mawasiliano ya kielektronikia (EPOCA) ya 2010 inayotoa
jukumu la muuzaji au mtumiaji wa simu kusajili namba
zao kabla ya kuitumia. Na usajili wa namba katika vituo
vyetu vya wasambazaji mawakala nchini nzima ni bure
aliongeza Singano
Chini ya kifungu cha 130 cha sheria ya posta na
mawasiliano ya kielektronikia (EPOCA) ya 2010 ni
marufuku kwa mtu yeyote kuuza namba ya simu kwa
mtu yeyote bila kuweka kumbukumbu za mtumiaji wa
namba hiyo.

About Syed Faizan Ali

Faizan is a 17 year old young guy who is blessed with the art of Blogging,He love to Blog day in and day out,He is a Website Designer and a Certified Graphics Designer.

0 comments:

Post a Comment