Kesi ya mauaji ya Padri Evarist Mushi imechukua sura mpya, kufuatia
Jaji wa Mahakama kuu ya Zanzibar, Mkusa Isaac Sepetu kujitoa baada ya
upande wa utetezi kuwasilisha ombi la mshatikiwa Omar Mussa Makame
kutokuwa na imani naye.
Akisoma uamuzi baada ya kupokea maombi ya
upande wa utetezi, ambayo yaliwasilishwa Julai 2 mwaka huu, Jaji Mkusa
amesema kwamba uamuzi wa mshtakiwa ni haki yake kwa mujibu wa sheria
lakini amesema hakubaliani na hoja zilizotolewa na Wakili Abdallah Juma
Mohamed.
Wakili Abdallah Juma Mohamed aliwasilisha hoja tatu,
akimtaka Jaji Mkusa ajiondoe katika kesi hiyo, kuutaka upande wa
waendesha mashtaka wapewe muda maalum wa kukamilisha upelelezi wa kesi
hiyo na kuwasilisha mahakamani ili kesi hiyo iweze kusikilizwa kwa muda
muafaka.
Akitoa uamuzi wake, Jaji Mkusa amesema hoja zote zilizowasilishwa hazina msingi wowote, na
kinachoonekana
kwa upande wa utetezi unajaribu kuiburuza mahakama ikiwemo kuchagua
Jaji wa kusikiliza kesi hiyo kwa vile hoja za kumtaka kujiondoa
hazikuzingatia mashiko ya kisheria.
Jaji Mkusa amesema suala la
mshtakiwa kunyimwa dhamana lipo wazi kwa mujibu wa sheria ambapo makosa
ya mauaji hayana dhamana lakini wakili wa utetezi wamekuwa akiwasilisha
ombi la kutaka mteja wake aachiwe huru kila wakati kesi inapotajwa
wakati jambo hilo limeshatolewa uamuzi zaidi ya mara tatu.
Jaji
Mkusa amesema baada ya uamuzi wake wa kujitoa, jalada la kesi hiyo
litarudishwa kwa Jaji Mkuu kwa ajili ya taratibu za kupangiwa Jaji
mwingine, na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti mosi mwaka huu.
Mtuhumiwa
Omar Mussa Makame anakabiliwa na shtaka la kumuua Padri Evarist Mushi
mnamo Febuari 17 mwaka huu katika eneo la Beitrasi kwa kumpiga risasi
kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha sheria namba 6 ya mwaka 2004 ya
mwenendo wa makosa ya jinai ya Zanzibar.
About Syed Faizan Ali
Faizan is a 17 year old young guy who is blessed with the art of Blogging,He love to Blog day in and day out,He is a Website Designer and a Certified Graphics Designer.
0 comments:
Post a Comment