Wahusika wanajulikana. Wametajwa mara nyingi na mbinu wanazozifanya kwa kutumia wasanii wa kizazi kipya na waigizaji almaarufu kama 'Bongo Movie'.
Inaudhi, inakera na inatuongezea chuki sana kwa serikali iliyo madarakani. Kaeni kimya na endeleeni kulichafua taifa, kuna siku mtatueleza yote. Au kwakuwa wahusika ni wanenu? Au kwakuwa wakuu wa juu ni wale waliowawezesha kuingia madarakani kisiasa?
Ndugu zangu, hii ni aibu kubwa kwa Taifa. Inasikitisha sana na inazidi kutuaibisha wengine tunaosafiri ng'ambo. Taifa kama halina rais, taifa kama halina Vyombo vya Dola. Ni upumbavu, ni ufedhuli na mtambue sasa tumechoka.
Mambo haya mlimchomekea mtoto wa Mengi, mambo haya mnawachomekea wanyonge wenye njaa kali na hadi mmeua vijana wetu kwa kuwabebesha mizigo michafu hivi!
0 comments:
Post a Comment