Ni huzuni kubwa sana kuona vijana wetu wa kitanzania waliopo jeshini kutumika kama chambo vitani katika nchi nyingine. Tanzania tusijifanye ni wazalendo wa nchi zingine wakati wenye nchi zao wenyewe hawazijali. Zipo namna nyingi bora zaidi za kuleta amani duniani kuliko kupeleka majeshi ya kupigana vita.
Mpaka sasa bado sijaona faida ya moja kwa moja kwa nchi yangu katika vita hivyo.
Tanzania kwa sasa imepeleka vikosi vyake katika nchi za DRC, Sudan nk.
Ninatoa ombi kwa serikali ya Tanzania kuwarudisha haraka askari wetu nyumbani waje kulinda mipaka yetu, misitu yetu, Tembo wetu, Makazi yetu, Mali zetu na maisha ya watanzania. Popote pale mtanzania mpenda Haki na Amani tuungane katika hili katika kupiga kelele na kushinikiza.
Source:Jamii Forums
0 comments:
Post a Comment