Wednesday, 17 July 2013

HATIMAYE IMESEMEKANA CHADEMA CHANASA SIRI ZA MIPANGO YA CCM


By on 04:14

CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA)
kimefanikiwa kunasa siri
za mipango ya hujuma
zilizokuwa zimeandaliwa
na Chama Cha Mapinduzi
(CCM) katika uchaguzi
mdogo wa udiwani katika
kata nne za Jiji la Arusha,
Habari kutoka vyanzo
mbalimbali vya
kuaminika, zimebainisha
kuwa CHADEMA katika
uchaguzi huo kilifanikiwa
kushinda kata hizo baada
ya kuvunja ngome ya CCM
iliyokuwa ikiongozwa na
Naibu Katibu Mkuu wa
CCM, Mwigulu Nchemba.
Kwa mujibu wa habari
hizo, mipango karibu yote
iliyokuwa ikifanywa na
CCM, ikiwemo halali na
haramu, ilivuja na kufika
mikononi mwa wapinzani
wao ndani ya muda mfupi
hata kabla ya utekelezaji.
Imedaiwa kwamba baadhi
ya watu waliokuwa katika
kambi ya CCM, waliamua
kwa siri kufichua mipango
hiyo na kuifikisha kwa
mahasimu wao kutokana
na kile kilichodaiwa
kuchoshwa kushiriki
katika mambo ya
kidhalimu..
Taarifa hizo maofisa
kadhaa wa CCM ambao
wamekuwa wakiratibu na
kusimamia mipango
karibu yote miovu dhidi
ya wapinzani, waliamua
kwenda kinyume na
makubaliano hayo, na
kwa njia ya siri
wakafanikiwa kutoa
mpango mzima
hadharani.
Mmoja wa maofisa wa
CHADEMA ambaye awali
alikana taarifa hizo, kabla
ya kukiri baada ya
kubanwa, amedai
zilifikishwa kwao na watu
wenye mapenzi mema na
nchi.
“Hata nasi awali
tulishangaa, lakini
tulilazimika kuziamini
baada ya kuzifanyia kazi
na kubaini kwamba
zilikuwa za kweli.
“Kwa mfano taarifa za
kuwepo kwa mipango ya
kutumbukiza kura bandia,
kununua shahada za
kupigia kura ilivuja
mapema nasi tukaamua
kuweka mitego kila
mahali tulipoambiwa,
kiasi cha kuwafanya
washindwe kutimiza
lengo lao,” alisema ofisa
huyo.
Habari zimezidi kufichua
kuwa, kambi hiyo ya CCM
ilianza kuyeyuka mapema
mchana wa Jumapili, siku
ambayo ilikuwa ya
uchaguzi, baada ya kuhisi
kuwa mambo yao
yamekwama kutokana na
viongozi na vijana wao
kuonekana katika maeneo
yote muhimu yaliyokuwa
yamepangwa na chama
hicho tawala kuendesha
hujuma zake.
Habari zimezidi kufichua
kuwa, kambi hiyo ya CCM
ilianza kuyeyuka mapema
mchana wa Jumapili, siku
ambayo ilikuwa ya
uchaguzi, baada ya kuhisi
kuwa mambo yao
yamekwama kutokana na
viongozi na vijana wao
kuonekana katika maeneo
yote muhimu yaliyokuwa
yamepangwa na chama
hicho tawala kuendesha
hujuma zake.
Chanzo kimoja cha habari
cha kuaminika
kimeliambia Tanzania
Daima kuwa ‘usaliti’ huo
wa baadhi ya watendaji
wa chama hicho tawala
umetokana na
kutopendezwa na mtindo
wa utendaji kazi za kisiasa
unavyoendeshwa na
Mwigulu na baadhi ya
viongozi wa juu wa chama
hicho tawala.
“Wameanza kuchoshwa
na siasa za majitaka
ambazo zimezidi
kulichafua taifa na
kuangamiza maisha ya
watu.
“Ni kweli tunataka
ushindi, lakini wengi
hawataki utokane na
kuumiza watu ambao
wana haki ya kuunga
mkono na kufuata chama
wanachotaka,” kimesema
chanzo hicho, ambacho
kimeomba jina lake
lisitajwe kutokana na
sababu za kiusalama.
Mbali na sababu hizo,
taarifa zimebainisha kuwa
sababu nyingine
zilizowafikisha baadhi ya
watendaji wa CCM kusaliti,
ni kasi ya CHADEMA
kuungwa mkono na
wananchi, pamoja na
vitisho, na vitendo vingi
vya ukatili ambavyo
viongozi na wanachama
wa chama hicho pinzani
wamekumbana navyo.
Hadi sasa, viongozi wakuu
wote wa CHADEMA
wameonja adha ya polisi
kwa kukamatwa, wengine
kupigwa na hata
kufikishwa mahakamani
kwa tuhuma mbalimbali.
“Tunao wanachama
waaminifu ambao wamo
ndani ya CCM na
wamekuwa sehemu
muhimu ya intelijensia ya
chama chetu,” alitoboa
mmoja wa maofisa wa
CHADEMA.

About Syed Faizan Ali

Faizan is a 17 year old young guy who is blessed with the art of Blogging,He love to Blog day in and day out,He is a Website Designer and a Certified Graphics Designer.

0 comments:

Post a Comment