Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es
Salaam limekanusha habari zinazosema kuwa wao walitaka kumpiga bomu
mbunge wa ubungo John Mnyika lakini likamkosa.
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda Kova,
DCP Ali Mnenge amesema, Jeshi hilo lilikuwa katika doria za kawaida na
hawakuwa na mpango wa kuzuia mkutano huo ila walitaka kujua kwanini
wamekusanyika bila kibali.
DCP Mnenge amefafanua kuwa wakati
wakiwa katika maongezi na mbunge huyo ili awatawanyishe wananchi hao,
Askari aliyekuwa amebaki garini alikuwa akipanga vitu vizuri na ndipo
bomu hilo la machozi lilipuka na mlio mkubwa kusikika.
Amesema hali hiyo ya mlipuko
ilisababisha waliokusanyika katika mkutano huo kuhisi wana lengo la
kumlipua na bomu kiongozi huyo wakati si kweli, pia ameongeza hakuna
hata mtu mmoja aliyejeruhiwa.

0 comments:
Post a Comment